SEHEMU C UANDISHI.
NECTA 2007-(CANDIDATE)
Qn5. Andika insha yenye maneno mia moja (100) kuhusu moja ya
mada zifuatazo:-
(a) Maandalizi
ya uchguzi mkuu wa Oktoba 2005.
(b) Upimaji wa
virusi vya ukimwi.
(c) Mwenda tazi
na omo marejeo ngamani.
NECTA 20080(BOTH)
Qn8. Muundo wa uandishi wa barua za kirafiki na barua za
kikazi ni tofauti. Thibitsha kauli hiyo.
Qn9. Manyanda akiwa mfanyakazi wa kiwanda cha korosho
Tanitaalipewa taarifa kuhusu ugonjwa wa baba
yake. Wewe kama Manyanda andika barua ya kuomba ruhusa. Anuani ya kiwanda ni S.L.P. 1030, Kibaha.
NECTA 2009. (CANDIDATE)
Qn8. Andika insha
yenye maneno 250 kuhusu moja ya mada zifuatazo:-
(a) Aisifiaye
mvua imemnyeshea.
(b) Elimu ya
msingi ina umuhimu wake katika jamii.
(c) Maradhi
yanavyorudisha nyuma maendeleo ya familia hatimaye Taifa.
(d) Kueleimika
kwa msichana ni kueleimika kwa jamii.
(e) Wanyama
pori.
Qn9. Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwako, unahitaji
marafiki kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo. Andaa kadi ya mwaliko ili kuwapa
taarifa rafiki zako.
NECTA-2010 (CANDIDATE)
Qn8. Eleza tofauti iliyopo kati ya hotuba na risala. Andika
hotuba kuhusu “Maji ni uhai.”
Qn9. Wewe kama afisa ununuzi, andika barua kwa mfanyabiashara
mashuhuri wa wilayani kwenu kuhusu agizo
la bidhaa.
NECTA-2011 (CANDIDATE)
Qn8. Andika insha isiyo ya kisanaa yenye maneno mia mbili na
hamsini 250 kuhusu mandhari ya shule yenu.
Qn9. Andika kumbukumbu za kikao cha wanafunzi kuhusu sherehe
ya kumuaga mkuu wenu wa shule aliyepata wadhifawa kuwa Afisa elimu wa Mkoa.
NECTA-2012 (CANDIDATE)
Qn8. Jifanye kuwa umepata barua ya mwaliko wa sherehe ya siku
ya kuzaliwa ya rafiki yako aitwaye Faraja Matata, itakayofanyika siku ya tarehe
10/10/2012. Kwa bahati mbaya siku tatu kabla ya sherehe umepatwa na safari ya
kikazi kuelekea mkoani Singida. Andika barua ya kumtaarifu rafiki yako kuwa
hutaweza kuhudhuria sherehe hiyo. Jina lako liwe Tumaini Baraka.
Qn9. Andika insha yenye maneno ysiyopungua mia mbili na
hammsini (250) na yasiyozidimia tatu (300) kuhusu umuhimi wa huduma za simi ya
mkononi.
NECTA-2013 (CANDIDATE)
Qn8. Wewe ni mfanya biashara mahsuhuri mjini Dodoma. Andika
barua ya kutuma bidhaa kwa mteja wako aitwaye Dunia Msimbo anayeishi Lindi.
Jina lako liwe Nyila Sasisha.
Qn9. Andika tangazo katika gazeti la Rai ukitoa taarifa
kuhusu kupotea kwa mwanao aitwaye Raha Karaha, jina lako liwe Furaha Machupa.
NECTA-2013 (PRIVATE)
Qn8. Wewe ni Kiranja mkuu wa shule ya Sekondari Kazamoyo
iliyoko Tanga, jina lako Uwezo Jitihada na unasoma kidato cha nne. Andika barua
kwa mkuu wa Shule ukiomba ruhusa ya kuhudhuria semina ya uelimishaji rika
itakayofanyika tarehe 10/11/2013 katika Shule ya Sekondari Tutafika iliyoko
Moshi. Barua yako ipitie kwa Mwalimu wa darasa.
Qn9. Jifanye wewe una elimu ya kidato cha nne, jina lako
Situmai Kasheshe unayeishi katika kijiji cha Songambele kilichopo wilayani
Mpanda. Tumia taarifa zilizomo kwenye tangazo lifuatalo lililotolewa kwenye
gazeti la Mwananchi tarehe 01/12/2013 kuandika barua ya maombi ya kazi.
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
KAZI: Karani Masijala
SIFA:
·
Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu masomo ya kiingereza na
Hisabati
·
Awe na uri usiozidi miaka 35
·
Awe mtanzania
·
Awe na ujuzi wa kompyuta
Barua ya
maombi iambatanishwe na nakala za vyeti na itufikie kala ya tarehe 15/12/2013.
Maombi yote
yatumwe kwa:
Afisa Mwajiri
Kampuni ya Kutengeneza
Masufuria
S.L.P 600
KATAVI
NECTA-2014
(BOTH)
Qn8. Andika
insha yenye maneno yasiyopungua mia mbili (200) na yasiyozidi mia tatu (300)
kuhusu methali isemayo “Samaki mkunje angali mbichi.”
Qn9. Wewe ni
mwenyekiti wa mtaa abao umekumbwa na mafuriko lakini wananchi wako wanakataa
kuhamia makazi mapya. Andika hotuba utakayoitoa kwa wananchi wa mtaa wako ili
kuwashawishi kuondoka katika sehemu hiyo. Jina la mtaa ni Kwamachombo na eneo
la makazi mapya linaitwa Kitivo.
0 comments:
Post a Comment