UTANGULIZI.
Sehemu hii inahuzsu usuli wa mada, ufafanuzi wa tatizo,
madhumuni ya utafiti, umuhimu wa itafiti, malengo ya utafiti na mapitio ya
utafiti.
USULI WA MADA.
Methali ni semi fupi fupi ambazo huwa na pande mbili ambapo
upande mmoja huanzisha wazo na upande mwengine hukamilisa wazo. Mfano: Mtaka
cha mvunguni sharti ainame. Methali kama utanzu mmoja wa fasihi simulizi una
nafasi kubwa sana katika jamii kwani utanzu huu huonya, huelimisha, hukosoa
pamoja na kubadilisha jamii.
Methali z imekuwa ni kipengele muhimu kutokana na kuundwa
kwa maelezomafupi sana na yenye ujumbe mzito.huvyo jamii huweza kunufaika
kutokana na urahisi wake katika kuzitumia.
Hata hivyo methali kwa upande mwengine huweza kupotosha
ikiwa zitaaeleweka vibaya ka wanajamii husika.
MADA YA UTAFITI.
Mada ya utaiti huu ni athari za matumizi ya methali katika
jamii
TATIZO LA UTAFITI
Wana jamii wengi wanatumia methali katika maisha yao ya kila
siku lakini inaonekana huzitumia kinyume na methali hizo.kwa hiyo ipo haja ya
kuzichunguza athari za matumizi mazuri na mabaya yamethali katika jamii .Ili
kuweza wana jamii kuzitumia methali katika mazingira yaliyo sahihi.
MALENGO YA UTAFITI
Kuchunguza athari za methali kwa watumiaji katika jamii
LENGO KUU
Kuonesha athari nzuri za methali kwa wanajamii.
Kuonesha athari mbaya za methali zitumiwazo na wanajamii
MASWALI YA UTAFITI
Ni athari gani zinazopatikana katika jamii kutokana
namatumizi ya methali ?
Ni athari zipi mbaya zitakazojitokeza ikiwa methali
zitatumika vibaya ?
Ni athari zipi nzuri zitakazopatikana katika jamii endapo
methali zitaeleweka vizuri
UMUHIMU WA UTAITI
Utafiti huu utatoa mwanga kwa jamii juu ya athari za
matumizimabaya ya methali katika jamii.vile vile utafiti huu uutachochea kuzuka
kwa tafiti nyegine zenye kengo la kuhifadhina kuendeleza methali katika jamii.
Na mwisho utafiti huuu utatumika kama marejeleo kwa watakaofanya utsiti
ENEO LA UTAFITI
Katika utafiti huu ttutachunguza athari za methali za
Kiswahili tu ambazo pia ni zile zinazopatikana katka Kiswahili sanifu, kwa
maana ya kwamba utaiti huuu haukugusa methali nyengine kama vile methali za
kilahaja, mfano: Kimakunduchi n.k.
MAPITO YA MAANDIKO.
Sura hii ilihusu mambo yaliyoandikwa kna watafiti mbali
mbali kuhusiana na mada hii.
Mapitio ya maandishi.
Miongoni wa vitabu na achapisho ambayo watafiti waliptia ni
Ngole na Honero (1981), Mbughuni (1982), Bakhresa (1993), Karama S (1994),
Mulokoz M.M (1996), Tuki (2004), Mbarouk, S.S (2005), Masebo, J.A na Nyangwine
(2008), Wanjala, F.S (2011).
Ngole na Hanero (1981), wameeleza maana ya methali kuwa “ Ni
aina ya usemi mzito ambao umekusudiwa kusema suala maalum, lakini kwa afumbo.
Usemi huu mzito mara nyingi hukusudiwa kuonya, kuongoza na kuadilisha
mwanadamu”. Kuktokana na maelezo ya
wataalaumu haawa nao pia wameonesha kwa uwazi kuwa methali huonya, huongoza na
huadilisha.
Mbughuni (1993) amesema “maadili huwa ni lile funzo
linalohusu maisha ya jamii na imani zake, misingi ya imani hiyo katika elimu,
uchumi, siasa na utaaduni, tabia, mila na desturi, malengo, madhumuni na mategemeo ys jsmiikuhusu hayo yote”.
Karama, S (1994) ameeleza maana yamethali na
matumizi yake na akaendelea kusema matumizi yaliyotolewa ni fano tu ili
kumfahamisha mtu lakini bila shaka ethali hiyo huweza kutumika kwa hali
nyemngine.
Mulokoz, M.M (1996) aansema kuwa “methali ni usemi mfupi wa
mapokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yanayotokana na
tajriba ya jamii ina yohusika”. Kwa mujibu wa m taalamu huyu ni dhahir kwamba methali hutumika katika malezi jambo
ambalo ni muhimu kwa jamiii.
TUKI (2004) “Methali ni mwenendo mwema, onyo au mafundisho
yatolewayo kwa njia ya hadithi au ushairi na yenye kufundisha mambo mazuri”
Maadili pia huweza kupatikana katika methali na hutumika katiika malezi.
Suleiman, A.S (2005) yeye amezigawa methali katika makundi tofauti, zikiwemo methali
zinazoonya, kuhimiza na kubadilisha. Pia ameeleza maana ya methali kuwa: “
Methali ni maneno mafupi ya hekima yenye kutoa ujumbe mzito kwa jamii.
Masebo, J.A na Nyangwine (2006) wamesisitiza kuwa “ Methali ni
utanzu tegemezi ambao kutokea kwake
hutegemea fani zingine. Kwa mfano maongezi ya majadiliano mazito katika
miktadha maalum ya kijamii./ baadhi ya methaliu huwa ni kielelezo au vofupisho
vya hadithi Fulani ianyofahamika kwa wanajamii”
Wamitila, K.W (2007) wamaesma kuwa “Methali hutumika kuonya,
kuelimisha na kukosoa:. Lakini hakutathmini matumizi ya methali katika kuonya,
kuelimisha na kukosoa.
Haji, A na wenzake
(2007) wamechamb ua maudhui ya ,methali kwa kuonyesha ujumbe na mafunzo
lakini hawakutathmini matumizi ya methali yanayoweza kutumika katika malezi.
Masebo, J.A na Nyangwine, N (2008) wameeleza kuwa “ Methali
ni semi fupi fupi zenye kueleza kwa
muhtasari, fikra au mafunzo mazito yanayotokana na uzoefu wa kijamii, mara
nyingi mawazo hayo huelezwa kwa kutumia tamaathali hasa sitiari naa mafumbo.”
Wajal, F.S (2011) anasema “ Methali ni semi fupi fupi
zinazosheheni fumbo juu ya ukweli juu ya maisha ya m wanaadamu na huwa na umbo
maalum. Semi hizi aghlabu huwa za kimapokeo kutoka kizazi hadi kizazi kwa
kawaida huwa na sehemu mbili, sehemu ya
kwanza huzua suala na sehemu ya pili hukamilisha suala hilo, pia huwa na lugha
teule inayoteuliwa kwa ustadi mkubwa.”
www.gat.Kosoft.com/swa/methali.15/5/2015.
nwameeleza kuwa “ Methali ni tungo mbili za kisanaa ambazo hutoa wasia-nasaha
kwa lugha ya mafumbo. Pia wamezungumzia sufa za methali, methali huwa na funzo, methali huwa na ukinzani.”
www.wikipedia.org/wiki/methali.155/2015.
Methali ni usemi mfupi wa mapokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra au mawazo
mazito yanayotokana na uzoefu wa maisha ya jamii husika. Pia methali ni kauli
fupi zenye pande mbili za fikra.
www.afriprov.org/indexphp/bibilioraphy/366-methalizakiutamaduni15
/5/2015. methali ni lugha nyepesi ipenyayo moja kwa moja katika nyoyo za
wasikilizaji. Aidha methali ni njia ya mkato ya kuelimisha, kukosoa hususan
vijana katika kuzingatia tunu za jadi kwa kina ndani ya mazingira ya asili ya
jamii.
Kutokana na maelezo wataalamu mbali mbali waliozungumzia
kuhusu methali za Kiswahili, inaonesha kuwa wapo waliozungumzia kuhusu nafasi ya
methali, muundo wa methali na matumizi ya methali lakini hawakutathmini matumizi ya methali za Kiswahili katika
malezi na kuacha pengo kubwa la kutathmini matumizi ya methali, hivyo utafiti
huu unakusudia kuziba pengo hilo.
MBINU ZA UTAFITI
Kipengele hiki kinazungumzia mbinu mbali mbali za utafiti
ambazo zilitumika katika ukkusanyaji wa data, utaratibu wa utafiti, vifaa vya
kukusanyia data, uchanganuzi wa data, kategoria ya waliohojiwa. Sababu za
uteuzi wa kategoria ya waliohojiwa.
UKUSANYAJI WA DATA
Utafiti huu ulitumia njia tofauti tofauti ili kufikia
malengo yaliyokusudiwa. Mbinu hizo ni maktabani na mahojiano.
MBINU YA MAKTABANI.
Mbinu hii ilhusisha usomaji wa machapisho mbali mbali
vikiwemo vitabu na machapisho mengine ambayo watafiti walipata taarifa
kulingana na mada yao ya utafiti. Mbinu hii ilichaguliwa kupata taarifa zaidi
juu ya utafiti wao.
VIFAA VYA KUKUSANYIA DATA.
Utafiti huu ulitumia vifaa mbali mbali kama vile kalamu,
karatasi, simu za mkononi, kompyuta na dodoso.
KATEGORIA YA WAHOJIWA.
Ni watu ambao walichaguliwa kushiriki katika utafiti. Katika
utafiti huu wazee, walimu, wanafunzi na vijana walihusishwa ili kutoa taarifa
kwa urahisi na kwa usahihi. Katika utafiti huu watafiti walitumia sampuli ya
makundi kwa kuteua baadhi ya wazee, vyama, walimu na wanafunzi, wataiti
walitumia sampuli hii kwasababu ndio iliyosaidia kupata data sahihi kulingana
na utafiti wao.
SABABU YA KUTEULIWA KATEGORIA YA WAHOJIWA
Katika sampuli hii ukusanyaji wa data uliumuisha jinsia zote
yaani wanawake na wanaume kama ifuatavyo:
SAMPULI YA
KATEGORIA YA WATAFITIWA/ WALIOHOJIWA
WATAFITIWA
|
WANAUME
|
WANAWAKE
|
ENEO
|
IDADI
|
ASILIMIA
|
WANAFUNZI
|
5
|
6
|
SKULI YA JANG’OMBE
|
13
|
|
WANAFUNZI
|
6
|
6
|
SKULI YA HAMAMNI
|
12
|
|
JUMLA
|
|
|
|
25
|
50%
|
WALIMU
|
2
|
6
|
SKULI YA JANG’OMBE
|
8
|
|
WALIMU
|
2
|
4
|
SKULI YA HAMAMNI
|
7
|
|
JUMLA
|
|
|
|
15
|
30%
|
WAZEE
|
4
|
6
|
KIPONDA
|
10
|
20%
|
JUMLA
|
20
|
30
|
|
50
|
100%
|
UCHANGANUZI WA DATA.
0 comments:
Post a Comment